Fasihi ni mtazamo halisi

13 10 2007

Ni maisha ni msukumo wa maisha ni matarajio ya maisha kwa uongozi wa awamu hii ambapo wananchi wamekata tamaa ya maisha yao kila umuonaye analalamikia kushuka kwa uchumi ndani ya mfuko wake,nini mustakabali wa hili nani anapaswa kulaumiwa?wananchi viongozi au mazingira ya nchi yenye rasilimali zenye utajiri na maskini?

Ni Ari Mpya ya maisha magumu ambayo kwayo wananchi kwa amuda usiozidi miaka miwili wamefikia hatua ya kudiriki mlo mmoja kwa siku na kutafakari namna ya kuupata mlo huo kwa siku nyingine, nini matumaini ya mdanganyika huyo aliyezoea kuishi kwa raha mustarehe wanawe wakila na kulala bila dhiki?

Nguvu Mpya ya maisha ambayo matarajio yake ni ndoto kufikia mafanikio kama ilivyoainishwa katika kampeni za kisiasa kabla ya kushinda kwa kishindo na kuvibwaga vyama ambavyo havina NGUVU MPYA ya kumiliki dola nini matumaini ya nguvu hizi ambazo kwazo wananchi wanaaanza kuona kuwa wanaumizwa kwa nguvu bila kuwekewa  dira mbadala?

Kasi Mpya ya kudidimia ki maisha toka uwezekano wa kumiliki nyumba hadi kufikia mahali pa kupanga,kumiliki kipando cha maana hadi kufikia mahali pa kushindwa hata kupata baiskeli, ni kasi mpya ya wadaganyika kwa zaidi ya miaka 40 ya UHURU na hebu basi wananchi waondokane na usingizi totoro ambao kwao walioamka huuza mali asili na rasilimali huku wengine wakiamka hukuta kila kitu kimeuzwa kwa wawekezaji, ni kasi mpya hiyo ya watendaji kuharibu mustakabali wa sera na nia nzuri ya serikali.

Huu ni mtazamo tu yoyote anaweza kuwa na mtazamo wake kwa namna ambavyo fikra zake zinamtuma kupanga na kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Ni mtazamo ulioshabihiana na fikra mbadala na kuacha ukiritimba uliogubika kuhodhi kila kilichopo kuwa mikononi wa watawala ambao wameacha kuongoza na kubeba UTAWALA.

Wakatabahu….Eid Mubarak 


Actions

Information

Leave a comment