Fasihi ni mtazamo halisi

13 10 2007

Ni maisha ni msukumo wa maisha ni matarajio ya maisha kwa uongozi wa awamu hii ambapo wananchi wamekata tamaa ya maisha yao kila umuonaye analalamikia kushuka kwa uchumi ndani ya mfuko wake,nini mustakabali wa hili nani anapaswa kulaumiwa?wananchi viongozi au mazingira ya nchi yenye rasilimali zenye utajiri na maskini?

Ni Ari Mpya ya maisha magumu ambayo kwayo wananchi kwa amuda usiozidi miaka miwili wamefikia hatua ya kudiriki mlo mmoja kwa siku na kutafakari namna ya kuupata mlo huo kwa siku nyingine, nini matumaini ya mdanganyika huyo aliyezoea kuishi kwa raha mustarehe wanawe wakila na kulala bila dhiki?

Nguvu Mpya ya maisha ambayo matarajio yake ni ndoto kufikia mafanikio kama ilivyoainishwa katika kampeni za kisiasa kabla ya kushinda kwa kishindo na kuvibwaga vyama ambavyo havina NGUVU MPYA ya kumiliki dola nini matumaini ya nguvu hizi ambazo kwazo wananchi wanaaanza kuona kuwa wanaumizwa kwa nguvu bila kuwekewa  dira mbadala?

Kasi Mpya ya kudidimia ki maisha toka uwezekano wa kumiliki nyumba hadi kufikia mahali pa kupanga,kumiliki kipando cha maana hadi kufikia mahali pa kushindwa hata kupata baiskeli, ni kasi mpya ya wadaganyika kwa zaidi ya miaka 40 ya UHURU na hebu basi wananchi waondokane na usingizi totoro ambao kwao walioamka huuza mali asili na rasilimali huku wengine wakiamka hukuta kila kitu kimeuzwa kwa wawekezaji, ni kasi mpya hiyo ya watendaji kuharibu mustakabali wa sera na nia nzuri ya serikali.

Huu ni mtazamo tu yoyote anaweza kuwa na mtazamo wake kwa namna ambavyo fikra zake zinamtuma kupanga na kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Ni mtazamo ulioshabihiana na fikra mbadala na kuacha ukiritimba uliogubika kuhodhi kila kilichopo kuwa mikononi wa watawala ambao wameacha kuongoza na kubeba UTAWALA.

Wakatabahu….Eid Mubarak 

Advertisements
Watendaji kwenye mfumo hujisahau, hudhani ni wao pekee

27 09 2007

KUNA wakati mtu husifiwa kwa sifa na utendaji bora asiostahili na akafika mahala akalewa sifa hizo ambazo hata hivyo si hirimu yake kadhalika hazina matunda ya utendaji bora.

Ulevi huu wa sifa isiyo stahili yake husababisha kutojiona amekosea na hivyo kukithirisha utedaji mbovu akidhani kuwa anatenda vyema ilhali machoni mwa jamii anazidi kuharibu.

Walio karibu yake huendelea kumpamba kwa sifa asizostahili na kumsifia kwa kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa huku wakimramba kichogo na wale waliojibari na himaya yake humdhania kuwa ni mahiri kwa utendaji kutokana na sifa lukuki asizostahili ambazo amevikwa nazo.

Wanapo tanabahi na kubaini asifiwayo hayakuwa stahili yake huanza kumbeza na kumuona si lolote si chochote ilhali awali walimuona ni mbuji na mahiri wa utendaji, kwani aliweza kusifiwa kwa sifa lukuki walizomdhania kuwa ni zake katika utendaji, mtendaji hulaaniwa na kubezwa.

Hatua hii inatokana na madhara ya kutofanya utafiti kabla ya kupewa mamlaka mtendaji huyo,maisha ya kufikirika na kusadikika ndio mfumo uliopo katika nchi ya Wadanganyika kwa karne na karne.

Kwa mtindo wa aina hii, maadui huongezeka siku hadi siku badala ya kupungua kutokana na msifiwa kuvikwa sifa si zake na hili ni tatizo ambalo limekuwa sugu miongoni mwa wananchi wanaotarajia maisha mema yenye kupatikana huduma zote muhimu za kijamii.

Rushwa,ukiritimba wa uongozi,ujambazi, kuhodhi mali za wananchi, mikataba mibovu ni miongoni mwa nyimbo ambazo kwa sasa hazina muimbaji, waimbaji wake wamefumba midomo wamekuwa mabubu, hawasemi,wamekuwa vipofu hawaoni, wamekuwa viziwi hawasikii, wamekuwa walemavu, hawatembei.

Hayo ndiyo maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kipindi kisichozidi hata miaka miwili!!! hata hiyo miaka mitano ka mujibu wa sheria zilizopo haijafika.

Namkumbuka muimbaji mahiri wa nyimbo za kifasihi, Mrisho Mpoto, pale alipoimba wimbo kwa kushirikiana na mwanadada IRENE Sanga, aliposema, ”Mmetupima viatu mwaka huu….baada ya miaka mitano mtakuja na kutuuliza hivi mlikuwa mnavaa viatu aina gani?

Si maneno tu ya nyimbo bali ni ujumbe mahsusi wa kifasihi ambao bila shaka wajomba wamepata ujumbe na hivyo wanachoatakiwa kukifanya ni kuufanyia kazi na kufanyia marekebisho matatizo yanayoizunguka jamii yetu.

Ni kawaida ya mtu kushirikiana na rafiki yake katika utendaji lakini si kila kitu unaweza kumshirikisha rafiki yako hata katika mambo nyeti yanayohitaji ufumbuzi wa kijamii,mtu yoyote ni lazima amsogeze rafikiye wa karibu katika utendaji unaomhusu binafsi lakini si katika utendaji unaolihusu Taifa.

Urafiki una mahali pake hasa rafiki akiwa naye ni mtendaji mzuri, anaweza kuwasaidia wananchi kwa kila hali, na iwapo rafiki si mtendaji, atakuwa katika nafasi ile ya uitendaji kwa matlaba yake na hivyo kuacha vilio kwa wanajamii na kumuona mtendaji mkuu anaboronga.

Hii ndiyo hali halisi iliyopo!!!! nachelea kusema matokeo ya haya ni kushindwa kukamilisha utendaji bora na wananchi kulaumu utendaji ulioshangiliwa kwa hoi hoi, vifijo na nderemo!!!!!miaka miwili iliyopita.

Ni ujumbe mahsusi kabisa huu ambao ni wajibu kwa mtendaji mahiri kujua mustakabali wake vinginevyoo…..vizazi vitapiga mboko makaburi yetu kwamba hata sisi tuliona kisha hatukusema lolote.

Alamsiki Bin Nuuur!!!!!

Hello world!

10 09 2007

Welcome to WordPress.com. This is your first post. Edit or delete it and start blogging!

Bilion 21 ni ukombozi ama viini macho???

23 12 2006

Naam ni mwaka mmoja wa Mheshimiwa JK, nini mustakabali wa SIHASA hapa nchini kwetu, ndio mwanzo wa kuua vyama vya upinzani au ndio chachu ya kuimarisha demokrasia?lakini ni vigumu kupima maendeleo ya nchi kwa siku 365-1/4 bali la muhimu kuangalia utekelezaji wake jee una manufaa kwa wananchi au ndo nyimbo hizo za kila siku za maisha bora kwa kila Mtanzania?.

Juzi nilikuwa katika kijiwe cha kahawa mahala fulani, kile nilichokisikia katika kijiwe kile kilinitia mshawasha wa kupandisha komenti hizi, katika kijiwe hicho nilisikia vijana wakishabikia Sh. Bilion 21 za serikali zilizotolewa kwa kila mkoa.

Nilimsikia kila mmoja akipanga bajeti na majukumu yake, mara baada ya kupata fedha hizo, kilichonishangaza na haswa kupata hamu ya kutoa fikra zangu ni baada ya kutafakari na kuona kuwa fedha hizo si lolote wala chochote,baada ya kutokea jamaa mmoja ambaye alianza kuzipigia hesabu fedha hizo kulingana na takwimu ya wahitaji.

Jamaa huyo alinipigia Sh. Bilion 21 ambazo ni sawa na Sh. Milion 1000 kwa kila mkoa ambao unatarajiwa kupata Sh. Milion 1, ambapo pia akapigia wastani wa wilaya tano na kupata kila wilaya inaweza kupata wastani wa Sh.Milion 200 ambapo pia akapigia kwa wastani wa kata 10 na kupata wastani wa kila kata moja kupata Sh. laki 5.

Kadhalika katika mahesabu yake alipigia wastani wa vijana 1000 kwa kila kata wakawa ni wahitaji wa fdha hizo akagawanya kwa laki tano akapata kiasi cha Sh.elfu tano kwa kila kijana pia akajaribu kuangalia bei ya mbolea kabla hajatolewa ruzuku ya serikali ya mfuko Sh.35,000, hapo ndipo nilipoachama mdomo na kusema kuwa huu ni usanii.

Nikajiuliza swali moja hivui serikali imefanya upembuzi wa kina kujua kama ni kweli hizo Milion 21 zinaweza kukiddhi mahitaji ya walalahoi na hivyo kuwa na maisha bora kwa kila Mtanzania nikagundua kuwa kuna usanii ulio wazi ambao kwa hakika mtu wa kawaida hawezi kubaini.

Ndugu zangu hii nchi ni yetu na sisi sote ni wahitaji wa kile kilichomo ndani ya nchi yetu, hivi ni kwa nini basi tuwe tunadanganywa kama watoto wadogo, tuangalie uhalisi wa maisha ya mwananchi wa kawadia ambaye aghalabu huambulia mlo mmoja kila siku na kutafakari namna ya kupata mlo kwa siku nyingine.

Maisha ya mtu wa aina hii ambaye elimu yake, afya yake, malazi yake pamoja na huduma za matibabu zinahitaji fedha anaweza kujikimu na kuishi katika anga hili na akajivunia kuwa yuko katika maisha bora?

Hili ni swali ambalo ninajiuliza binafsi na kila mmoja anaweza kuwa na wazo lake binafsi, na tuangalie kama ni kweli tuko katika mapambano ya umaskini kuelekea sera kuelekea 2025 kama inavyoeleza sera ya Taifa ya kukuza uchumi na kuondosha umaskini MKUKUTA.

Wakatabahu

30 11 2006

Binadamu na mtu yote ni majina ambayo amepewa kiumbe aliyeumbwa na na Mola na kupewa utashi wa kujua zuri na baya na kumaizi yanayojiri kwa matlaba ya kuishi vyema na vimbe wa aina yake na wale wanaoshabihiana naye katika dunia.

Ni jambo la aibu kuona binadamu anauvua utu wake na kudiriki kujamiina na binadamu mwenzie kinyume na maumbile ambapo si hivyo tu bali binadamu hao wamevuka hali ya ubinadamu na kujivika unyama na kwa kujamiina na wanyama seuze watoto wadogo vichanga…inatia aibu.

Huwa nakaa na kutafakari hatima ya sisi tunaojiita binadamu wenye utu kwa vitendo hivi vinavyozidi unyama,haya mambo asili yake ni wapi na ni kwa nini uwepo unyama wa aina hii.

Limekuwa ni jambo la kawaida kila uchao kusikia mara ooh! babu fulani kambaka binti mdogo mwenye umri wa miaka miwili au minne tena pia si ajabu kusikia kwamba kuna mtu kabambwa akimpanda kuku au ng’ombe,hata kule Mbozi mkoani Mbeya ilipata kutokea jamaa akatengeneza jiwe lililoshabihiana na maumbile ya sehemu za siri za mwanamke na kutumia fursa hiyo kuliingilia jiwe hilo na hatimaye kupata madhara katika sehemu zake za siri.

Jamaa huyo ilidaiwa alifanya hivyo kwa ajili ya kujilinda na ugonjwa wa UKIMWI lakini je ni kweli inakuja akilini kwamba aliyefanya kitendo kile ana akili timamu?tunaweza kumsifu jamaa huyo lakini hebu na tujiulize hii amri ya watawa kutoolewa na kutooa ina madhara gani kwa jamii?

Naamini maumbile ya binadamu huenda kulingana na jinsi Mwenyezi Mungu alivyotaka yawe sasa iwapo kuna baadhi ya madhehebu yanashiniza watu wasioe au kuolewa nini mantiki yake hapa, inawezekana hili jambo ndilo linaloshawishi vitendo vya kinyama vikashamiri

Wakatabahu kazi kwenu wachangiaji

30 11 2006

Binadamu na mtu yote ni majina ambayo amepewa kiumbe aliyeumbwa na na Mola na kupewa utashi wa kujua zuri na baya na kumaizi yanayojiri kwa matlaba ya kuishi vyema na vimbe wa aina yake na wale wanaoshabihiana naye katika dunia.

Ni jambo la aibu kuona binadamu anauvua utu wake na kudiriki kujamiina na binadamu mwenzie kinyume na maumbile ambapo si hivyo tu bali binadamu hao wamevuka hali ya ubinadamu na kujivika unyama na kwa kujamiina na wanyama seuze watoto wadogo vichanga…inatia aibu.

Huwa nakaa na kutafakari hatima ya sisi tunaojiita binadamu wenye utu kwa vitendo hivi vinavyozidi unyama,haya mambo asili yake ni wapi na ni kwa nini uwepo unyama wa aina hii.

Limekuwa ni jambo la kawaida kila uchao kusikia mara ooh! babu fulani kambaka binti mdogo mwenye umri wa miaka miwili au minne tena pia si ajabu kusikia kwamba kuna mtu kabambwa akimpanda kuku au ng’ombe,hata kule Mbozi mkoani Mbeya ilipata kutokea jamaa akatengeneza jiwe lililoshabihiana na maumbile ya sehemu za siri za mwanamke na kutumia fursa hiyo kuliingilia jiwe hilo na hatimaye kupata madhara katika sehemu zake za siri.

Jamaa huyo ilidaiwa alifanya hivyo kwa ajili ya kujilinda na ugonjwa wa UKIMWI lakini je ni kweli inakuja akilini kwamba aliyefanya kitendo kile ana akili timamu?tunaweza kumsifu jamaa huyo lakini hebu na tujiulize hii amri ya watawa kutoolewa na kutooa ina madhara gani kwa jamii?

Naamini maumbile ya binadamu huenda kulingana na jinsi Mwenyezi Mungu alivyotaka yawe sasa iwapo kuna baadhi ya madhehebu yanashiniza watu wasioe au kuolewa nini mantiki yake hapa, inawezekana hili jambo ndilo linaloshawishi vitendo vya kinyama vikashamiri

Wakatabahu kazi kwenu wachangiaji

Matunda ya Ari Mpya na Nguvu mpya bila fikra mpya

13 11 2006

Nilitaka kusema, nikashikwa na kigugumizi lakini hata hivyo nilijikuta nasema ingawa nikashikwa mdomo na sheria ya kutoingilia mahakama, bali nadhani hakuna mahakama inayofanya kazi zake kisheria kufuata maoni na vishawishi vya watu wa mitaani.

Naamini mahakama zote zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na zinatoa haki kulingana na makosa husika bila kufuata ushawishi wa chombo chochote au maoni ya watu wa mitaani.

Hapa nina nia ya kulisema jambo hili ambalo magazeti ya Tanzania yamelivalia njuga kwa kipindi hiki ambacho serikali imepania kupigania haki za wanyonge kwa nguvu mpya kasi mpya na ari mpya.

Maskini Bro.Dito mtoto wa Ramadhani Mwinshehe wa Mzuzuri Born Town kitendo kilichomfika kinataka kuingia katika mkumbo wa kisiasa sijui kwa kuwa naye ni kijana kada aliyelelewa na siasa na kufika hapo alipo inasikitisha bali inaumiza familia ya Bin Mbonde ambaye amepoteza uhai wake bila hatia.

Hakustahili kuuawa bali sheria ya usalama barabarani ingefuatwa lakini si kama vile ilivyotokea kwa kiongozi mkuu kama Bro.Dito kuchomoa bastola na kumlenga shabaha dereva wa daladala kichwani.

Sijui ilikuwaje na wala sitaki kufikiria jinsi ilivyokuwa patashika kwaabiria waliokuwa wakiendeshwa na marehemu Mbonde wakati huo, mie nadhani walihisi basi limevamiwa na majambazi ambao hatimaye huenda wangeamrishwa kulala chini na kuvuliwa nguo zao.

Mie nadhani kilichofanyika hakikudiriki hasira kiasi hicho, au basi mkuu huyo angepiga risasi magurudumu ya gari lisiende mbele na hatimaye dereva angeshuka chini, bali kilichofanyika kwa kitendo cha kulipita gari kisha kulizuia lisiende na Mzee Dito kushuka kunako gari na kutoa cha moto.

Inatisha na nachelea kuendelea kusema kwa kile nilichokisema awali tumefungwa mdomo na sheria tuiache mahakama itende haki!!!!!!!!!

Ilianza kwa mkuu wa wilaya kumpiga mwenyekiti vibao, ikaja kwa RPC kuwatandika viboko wananchi imekuja kwa RC kuchomoa bastola na kumuua dereva wa daladala, itakuwaja kwa Waziri sijui atafanya nini….. na nanihii atafanya nini na nani hii atafanya nini mwishowe watu wataamua kujitoa muhanga ni hatari haki isipotendeka huu ni mtazamo wangu sidhani kama sheria inaweza kufuata mtazamo wa mtu na kuufanyia kazi.